• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wafanya biashara wa madini wabuni njia ya kukwepa kodi

  (GMT+08:00) 2018-02-09 19:09:57

  Wafanyabiashara wa madini ya tanzanite na wamiliki wa migodi katika mikoa ya Arusha na Manyara, wamebuni njia haramu ya kukwepa kulipa kodi ya serikali kwa kufanya biashara ya madini hayo, kwa njia za wizi.

  Wafanyabiashara hao wameamua kuunda vikundi vya wachimbaji wadogo, maarufu kwa jina la 'WanaApollo' ili kuchimba kwa njia ya wizi katika Mgodi wa Kitalu C, unaomilikiwa na wawekezaji wazawa, Sky Associates Limited na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (Stamico).

  Tayari wafanyabiashara watano na WanaApollo 14, wamekamatwa kutokana na wizi huohuku maofisa wa usalama wakiendelea na uchunguzi wa wizi huo, unaoinyima serikali mapato.

  Septemba mwaka jana, Rais John Magufuli aliagiza idara ya polisi kujenga ukuta wa kuzunguka vitalu vya kuanzia A hadi D vyenye madini ya tanzanite katika eneo la Mirerani, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara ili kudhibiti uchimbaji na biashara ya madini hayo.

  Rais Magufuli pia ameitaka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kushiriki katika ununuzi wa madini hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako