• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Muungano wa watengenezaji vileo wateta kuhusu bidhaa ghushi

  (GMT+08:00) 2018-02-09 19:11:07

  Muungano wa watengenezaji vileo hapa nchini (Abak) umeteta kuwa biashara haramu ya kughushi bidhaa za vileo vimejipa asilimia 50 ya soko hivyo basi kuhatarisha biashara halali katika sekta hiyo.

  Muungano huo umesema kulingana na jinsi hali ilivyo huenda biashara hiyo haramu ikathibiti asilimia 60 ya soko hilo la vileo kabla ya mwaka wa 2020.

  Kupitia barua kwa kitengo cha kupambana na bidhaa ghushi hapa nchini, msemaji wa muungano huo, Mohan Galot anasema kuwa ikiwa serikali haitapata jibu la kukabiliana na bidhaa hizo ghushi katika sekta hiyo, basi uchumi utakosa kuafikia malengo yake ya kukusanya ushuru wa kufadhili ajenda zake za kimaendeleo na hatimaye wafanyakazi watapoteze ajira kwa wingi.

  Hivi majuzi mwenyekiti wa Abak, Gordon Mutugi amesema kuwa asilimia 50 ya soko la pombe limethibitiwa na bidhaa ghushi na akaonya kuhusu hatari iliyoko kwa wateja na pia kwa uchumi.

  Malalamishi hiyo yanakuja wakati ambapo taarifa zinaonyesha kuwa uchumi wa Kenya unapoteza Sh1 bilioni kwa mwezi mikononi mwa sekta hiyo ya mivinyo bandia na ya kuiga bidhaa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako