• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kuhimiza maendeleo ya biashara ya kimataifa kwa mtandao wa Internet

  (GMT+08:00) 2018-02-09 19:34:11

  Mkurugenzi wa idara kuu ya forodha ya China Bw. Yu Guangzhou leo amesema kuwa, China itashirikiana na jumuiya ya kimataifa kufanya juhudi katika utungaji wa kanuni, matumizi ya sayansi na teknolojia pamoja na sekta nyingine, ili kuhimiza zaidi maendeleo ya biashara ya kimataifa kwa mtandao wa Internet.

  Bw. Yu Guangzhou amesema kuwa, biashara ya kimataifa kwa mtandao wa Internet ni daraja kati ya watumiaji na wazalishaji wa dunia nzima, pia ni nguvu ya kuvunja kujilinda kibiashara na kuhimiza biashara huria. Hivi sasa, China inashirikiana na nchi wanachama wengine wa shirika la forodha duniani kutunga mfumo wa kigezi cha biashara ya kimataifa kwa mtandao wa Internet, kukamilisha zaidi kanuni ya usimamizi na mpango wa utatuzi unaoweza kueneza zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako