• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ziara ya mjumbe wa taifa wa China nchini Marekani ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa pande mbili

  (GMT+08:00) 2018-02-11 15:01:51
  Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Lu Kang amesema ziara ya hivi karibuni ya mjumbe wa taifa wa China Yang Jiechi nchini Marekani itasaidia kupanga mpango wa mawasiliano na ushirikiano wa pande mbili katika siku za baadaye.

  Bw. Lu amewaambia waandishi wa habari kuwa ziara ya siku mbili ya Yang imewezesha pande hizo mbili kubadilishana maoni kuhusu uhusiano wao na masuala muhimu ya kimataifa na kikanda yanayofuatiliwa kwa pamoja. Amesema wakati wa ziara hiyo, pande hizo mbili zilitangaza kufanya raundi ya pili ya Mazungumzo ya Diplomasia na Usalama na Mazungumzo Mapana ya Uchumi katika nusu ya kwanza ya mwaka huu.

  Ameongeza kuwa wakati wa ziara hiyo, Bw. Yang alikutana na rais Donald Trump wa Marekani, waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson, mshauri wa usalama wa kitaifa H.R. McMaster na maofisa wengine muhimu.

  katika mikutano hiyo Bw. Yang alisema kuwa maendeleo yamepatikana katika uhusiano wa pande mbili katika miaka kadhaa iliyopita chini ya uongozi wa marais wa nchi hizo mbili, ambao walikubaliana kwenye mkutano wao uliofanyika hapa Beijing mwezi Novemba mwaka jana kuwa China na Marekani zina maslahi mapana ya pamoja na zina wajibu muhimu wa kulinda amani, ustawi na utulivu wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako