• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuchukua nafasi kubwa ya kiujenzi katika ukarabati mpya wa Syria

    (GMT+08:00) 2018-02-12 08:07:01

    Balozi wa China nchini Syria Qi Qianjin amesema, China itachukua nafasi kubwa katika na mchakato wa ukarabati na maendeleo ya Syria kwa kupitia misaada.

    Akizungumza wakati alipotembelea Hospitali ya Chuo Kikuu cha al-Muwasat mjini Damascus, balozi Qi amesema China itafanya hivyo kwa kutoa misaada zaidi kwa serikali na watu Syria, na kwamba China imetoa misaada mingi kuunga mkono sekta ya afya nchini Syria, ikiwemo ufadhili wa mradi wa ukarabati katika kitengo cha dharura kwenye hospitali hiyo uliohusisha kubadilisha nyaya za umeme, mabomba ya maji, lifti, kuongeza vitanda na vifaa vya matibabu.

    Balozi Qi amesema, anatumai kuwa msaada wa China utasaidia kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi wa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako