• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Shirikisho ya Somalia na viongozi wa majimbo wakubaliana kushughulikia masuala mbalimbali

  (GMT+08:00) 2018-02-12 08:11:24

  Viongozi wa kisiasa nchini Somalia jana walimaliza mkutano wa siku nne mjini Mogadishu, uliokuwa na lengo la kushughulikia masuala ya usalama, muongozo wa kisiasa wa mwaka 2020 na kugawana sawa rasilimali za taifa.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo, viongozi hao, kutoka serikali kuu na serikali za majimbo, walikubaliana kuongeza kasi ya mafungamano na mafunzo ya vikosi maalumu vya Danab ili kusaidia kutimiza utulivu nchini humo. Serikali pia imekubaliana kuunga mkono polisi wa majimbo na vikosi vya jeshi kwa kuwapatia silaha, mafunzo, mafao na vifaa.

  Mkutano huo pia umeipa kazi kamati ya usalama kutoa mpango wa bajeti kwa ajili ya ofisi za usalama za wajumbe wa serikali ya shirikisho. Mkutano huo uliohudhuriwa na rais Mohamed Abdullahi Farmajo, waziri mkuu Hassan Ali Khaire na viongozi wa majimbo, umekubali kugawa kwa usawa mapato kutoka makampuni ya kigeni ya uvuvi kwenye maeneo ya maji ya Somalia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako