• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Algeria na Marekani zajadili tishio la wapiganaji wa IS wanaorudi barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-02-12 08:54:58

  Algeria na Marekani zimejadili tishio linalotokana na wapiganaji wa kigaidi wanaorudi barani Afrika baada ya kushindwa kwa kundi la IS nchini Iraq na Syria.

  Waziri wa mambo ya nje wa Algeria Bw. Abdelkader Messahel amekutana na naibu mratibu mkuu wa mapambano dhidi ya ugaidi katika wizara ya mambo ya nje ya Marekani Bi. Alina Romanowski ambaye yuko ziarani nchini Algeria, na wamejadiliana kuhusu ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwenye mapambano dhidi ya ugaidi, pamoja na kanda ya Sahel barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako