• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ndege ya abiria ya Russia yaanguka karibu na Moscow

    (GMT+08:00) 2018-02-12 09:03:49

    Shirika la habari la Interfax limesema ndege moja ya Russia iliyokuwa na watu 71, wakiwemo abiria 65 na wafanyakazi 6, ilianguka jumapili dakika chache baada ya kuruka kutoka Moscow, na watu wote waliokuwa kwenye ndege hiyo walifariki dunia.

    Ndege hiyo aina ya Antonov-148 ya Shirika la ndege la Saratov ilianguka ikiwa njiani kutoka Moscow kuelekea Orska kwenye eneo la Orenburg, magharibi mwa Russia.

    Rais Vladimir Putin wa Russia ametoa salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa kwenye ajali hiyo, na kutoa amri ya kuunda tume ya serikali kuchunguza ajali hiyo ili kujua chanzo chake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako