• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yasema robo ya watoto wa Iraq wanaishi maisha duni

    (GMT+08:00) 2018-02-12 09:55:47

    Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limetoa taarifa ikisema vita dhidi ya kundi la Islamic State iliyoanza mwaka 2014 nchini Iraq imefanya robo ya watoto nchini humo waishi katika hali duni.

    Taarifa hiyo imesema, watoto milioni 3.7 wa Iraq waliangukia kwenye umaskini ,huku wengine zaidi ya milioni 3 wakikosa elimu au kuacha shule kutokana na vurugu na machafuko nchini humo.

    Takwimu zilizotolewa na UNICEF zinaonesha kuwa, kutokana na mashambulizi mengi yaliyotokea dhidi ya taasisi za elimu nchini Iraq tangu mwaka 2014, zaidi ya nusu ya shule nchini humo zinahitaji ukarabati. Shirika hilo pia limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia kujenga upya miundombinu wanayohitaji watoto, na kutoa huduma za umma kwa watoto nchini Iraq.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako