• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Shirikisho Afrika; Simba ya Tanzania na APR ya Rwanda zashinda kwa magoli 4-0 kila moja

  (GMT+08:00) 2018-02-12 09:56:19

  Simba ya Tanzania na APR ya Rwanda jana zimepata matokeo ya kufanana, ya ushindi wa magoli 4-0 katika mechi za awali za mashindano ya kombe la Shirikisho la soka barani Afrika.

  Jijini Dar es Salaam Simba ilishinda kwa magoli 4-0 ilipocheza dhidi ya Gendarmerie National ya Djibouti, na wafungaji wa magoli hayo muhimu kwa Samba ni Said Ndemla, John Boko aliyefunga mawili na Emmanuel Okwi.

  APR yenyewe ikiwa nyumbani mjini Kigali iliifunga Anse Reunion ya Shelisheli na ushindi huo ulichagizwa na magoli matatu yaliyofungwa na Djihad Bizimana na goli moja linguine likifungwa na Issa Bigirimana.

  Lakini Visiwani Zanzibar wenyeji Zimamoto katika mchuano hiyo walipata matokeo ya sare ya goli 1-1 na wageni wao timu ya Welayta Dicha ya Ethiopia.

  Nchini Kenya, AFC Leopards imetoshana nguvu kwa sare ya kufungana goli 1-1 na FOSA Juniors FC ya Madgascar kwenye mechi iliyopigwa mjini Kakamega, ambapo goli la AFC lilifungwa na Prince Papa Arko katika dakika ya tatu, lakini FOSA walisawazisha kunako dakika ya 15 kupitia Rado Mbolasoa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako