• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Timu ya Taifa ya Uganda yaendelea kujipima kwa ajili ya michezo ya kufuzu kombe la dunia

  (GMT+08:00) 2018-02-12 09:59:17

  Timu ya Taifa ya Uganda ya mchezo wa mpira wa kikapu Silverbacks jana imefungwa kwa pointi 69-67 na timu teule iliyoundwa na wachezaji kutoka timu mbalimbali za ligi kuu, katika mechi iliyofanyika kwenye uwanja wa Lugogo.

  Mechi hiyo ilikuwa moja ya michezo maalum ya kujiandaa na mashindano ya kufuzu kombe la dunia yatakayofanyika kuanzia tarehe 23 hadi 25 baadaye mwezi huu.

  Kocha mkuu wa timu hiyo Mandy Jurumi amesema licha kuwa pungufu kwa pointi kadhaa, mechi hiyo imetoa taswira ya muungano wa kitimu ambalo ndilo lilikuwa lengo lake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako