• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wapinzani wa jadi wa ligi kuu Polisi na Butali watunishiana misuli kwa sare ya goli 1-1

  (GMT+08:00) 2018-02-12 09:59:17

  Mabingwa wapya wa ligi ya mchezo wa mpira wa magongo nchini Kenya, timu ya Polisi jana imelazimishwa sare ya goli 1-1 na wapinzani wao wa kihistoria kwenye mchezo huo nchini Kenya Butali Sugar Warriors katika mechi yao ya mwisho ya ligi msimu.

  Katika mechi hiyo iliyofanyika mjini Nairobi, Polisi walikuwa wa kwanza kupata goli kupitia Amos Barkbir katika dakika ya 23 ambalo hata hivyo halikudumu kwani Warriors walisawazisha kupitia Seth Oburu.

  Sare hiyo haikuwa na madhara kwa Polisi kwa tayari walishatangazwa kuwa mabingwa wa kombe hilo mwezi uliopita na sasa wamefikisha pointi 77 kileleni mwa msima wa ligi hiyo, wakifuatiwa na Butali ambao hata hiyo nao wamefuzu kwa ajili ya mashindano ya Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako