• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maambukizi ya mafua nchini China yameshuka hadi kwenye kiwango cha chini

  (GMT+08:00) 2018-02-12 16:10:32

  Serikali ya China imeweka kipaumbele kwa kazi za kudhibiti mlipuko wa maambukizi ya ugonjwa wa mafua na hivi sasa, maambukizi hayo yameshuka hadi kwenye kiwango cha chini katika mikoa mbalimbali nchini humo.

  Naibu mkurugenzi wa Kamati ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China Bw. Wang Hesheng amesema, wakati sikukuu ya Spring inapokaribia, Kamati hiyo imepanga kwa mara nyingine kazi za kuzuia na kutibu maradhi ya kuambukiza katika majira ya baridi na mchipuko ili kuhakikisha wagonjwa wanapata matibabu kama kawaida hospitalini.

  Wakati huohuo, Bw. Wang amesema viashiria mbalimbali muhimu vya afya vya China vimezidi kiwango cha wastani cha nchi zenye kipato cha kati na juu, na kwamba mwaka jana, vifo vitokanavyo na ujauzito nchini China vilikuwa 19.6 kwa kila laki 1, na vifo vya watoto wachanga vilikuwa 6.8 kwa kila elfu 1.

  Mwaka jana, jarida maarufu la afya la The Lancet lilitangaza orodha ya upatikanaji na ubora wa matibabu kwa nchi na sehemu 195 duniani, na China ilikuwa moja kati ya nchi tano zinazopiga hatua kubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako