• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano kuhusu ukarabati wa Iraq waanza nchini Kuwait

  (GMT+08:00) 2018-02-12 16:13:06

  Mkutano wa kimataifa wa Kuwait kuhusu ukarabati wa Iraq umefunguliwa leo katika mji mkuu wa nchi hiyo Kuwait, na utafuatilia ukarabati wa Iraq baada ya vita na masuala muhimu husika.

  Mkutano huo wa siku tatu unaoshirikisha nchi kadhaa kubwa za kiuchumi, na mashirika ya kikanda na ya kimataifa, utatathmini msaada unaohitajika katika ukarabati wa Iraq baada ya vita iliyodumu kwa miaka mingi.

  Mkutano huo pia utajadili masuala mengine muhimu kuhusu maendeleo ya Iraq, ikiwemo ushiriki wa sekta binafsi kwenye mchakato wa ukarabati wa nchi hiyo.

  Mkutano huo utaendeshwa kwa pamoja na Kuwait, Iraq, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya na Benki ya Dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako