• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe Mnangagwa ameanza ziara rasmi nchini Botswana

  (GMT+08:00) 2018-02-12 18:53:43

  Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa ameondoka Harare kwenda Gaborone, Botswana, leo asubuhi ikiwa ni ziara yake ya kwanza rasmi tangu achukue madaraka kutoka kwa rais wa zamani Robert Mugabe Novemba mwaka jana.

  Chombo cha habari cha taifa New Ziana, kimeripoti kuwa Mnangagwa atajumuika na mawaziri wengine kadhaa ambao tayari wameshafika Botswana kwaajili ya mkutano kati ya pande hizo mbili. Rais wa Botswana Seretse Khama Ian Khama, ambaye alikuwa na uhusiano mbaya na Mugabe kwa kudai alishindwa kuendesha utawala wa sheria, ni miongoni mwa viongozi wa kikanda walioshuhudia Mnangagwa akiapishwa kama rais.

  Waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa wa Zimbabwe Sibusiso Moyo amesema ziara hiyo nchini Botswana itasukuma mbele uhusiano wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako