• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Jeshi la Afghanistan lagundua mabomu na maghala mawili ya silaha

  (GMT+08:00) 2018-02-12 19:01:25

  Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema Jeshi la Taifa la Afghanistan (ANA) limegundua mabomu ya kienyji na mabomu ya ardhini 76 ndani ya saa 24 zilizopita, na maghala makubwa mawili ya silaha hatari katika wilaya ya Ahmad Khil ya mashariki ya jimbo la Paktia.

  Wizara hiyo imebainisha kwamba yakiwa na risasi na silaha mbalimbali, maghala hayo ni ya kamanda wa mtandao wa Haqqani Bw. Gul Noor.

  Wanajeshi wameweka kizuizi ili kuhakikisha usalama wa eneo la tukio kabla ya kusafirishwa kwa risasi hizo.

  Jeshi la kitaifa linaendela kufanya juhudi ya kuhakikisha usalama wa jamii na Waafghanistan nchini kote.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako