• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya Afueni kwa wakulima baada ya serikali kupunguza bei ya mbolea

  (GMT+08:00) 2018-02-12 20:14:21

  Serikali imenunua tani 100,000 za mbolea na bei yake imepunguzwa.

  Bei mpya ya mbolea kwa wakulima ni Sh 1,200 kwa mfuko wa 50kg kutoka Sh1,800.

  Katibu wa Kilimo Richard Lesiyampe amesema mbolea ya mimea zishaanza kusafirishwa kutoka bandari ya Mombasa hadi Bodi ya Taifa ya Nafaka na Mazao tayari kwa msimu wa kupanda.

  Msimu wa uliopita serikali ilikuwa inauza mbolea sh 1,800 lakini msimu huu, bei hiyo imepungua kwa asilimia 33.3.

  Hii ni agizo kutoka kwa Rais kupunguza bei ili wakulima wengi waweze kununua mbolea na kuongeza uzalishaji.

  Lesiyampe amesema mbolea hiyo itagawanywa kwa wakulima zaidi ya milioni mbili waliosajiliwa msimu wa mvua refu unayotarajiwa kuanza katikati ya mwezi ujao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako