• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwenyekiti wa mkutano wa baraza kuu la UN asisitiza umuhimu wa kuzuia mapambano

    (GMT+08:00) 2018-02-13 08:52:35

    Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Bw. Miroslav Lajcak amesisitiza umuhimu wa kuzuia mapambano kwa ajili ya kulinda amani.

    Bw Lajcak amesema hayo aliposhiriki kwenye ufunguzi wa mkutano wa Kamati Maalumu ya Operesheni za Kulinda Amani ya Baraza Kuu hilo. Amesema Umoja wa Mataifa ulianzishwa ili kuwaokoa watu kutoka kwenye mateso ya vita, na sio kufanya mateso.

    Ameongeza kuwa kuzuia mapambano hakumaanishi kupunguza nguvu ya kulinda amani. Kazi ya kulinda amani inasaidia sana mchakato wa kisiasa na upatanishi, pia inaweza kuzuia mzizi wa mapambano. Aidha, amesema njia shirikishi pia inahitajika kwenye kazi ya kulinda amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako