• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vyombo vya habari Zanzibar vyapongezwa kwa ushirikiano mzuri na serikali

  (GMT+08:00) 2018-02-13 08:57:15

  Vyombo vya habari nchini Zanzibar vimepongezwa kwa ushirikiano mzuri na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwafikishia wananchi habari za kiuchumi na maendeleo.

  Katika mkutano na waandishi wa habari juzi katika ukumbi wa zamani wa baraza la wawakilishi Kikwajuni Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano na Habari Ikulu Ndugu Hassan Khatib Hassan aliwapongeza wanahabari kwa jinsi walivyowahabarisha wananchi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.

  "Nitoe shukrani kwa habari nzuri ambazo zimepatikana kwa niaba ya ofisi yetu katika maadhimisho ya miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.Mtakumbuka na mlikuwa mashuhuda viongozi wa serikali akiwa mwenyewe mMheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Barza la mapinduzi walikuwa ni wageni rasmi katika matukio mbalimbali.Sherehe tunaambiwa zilifana sana,taarifa zote zinaeleza hivyo,na sherehe zile haziwezi kufana sana bila ya mchango wa vyombo vya habari"

  Aidha Mkurugenzi huyo alitoa pongezi kwa wanahabari kwa kazi nzuri wanayoifanya,jambo ambalo linafanya serikali kufuatilia changamoto zozote zinazotangazwa na vyombo vya habari,na kuzitafutia ufumbuzi.

  "Mara nyingi tunaposikia taarifa kupitia vyombo vya habari,au kusoma au kuona,ile ndio inmayotupa sisi hatua ya kujua tuko wapi,wapi kuna nini,na nini kifanyike kama kuna changamoto kuweza kuzipatia ufumbuzi.Hayo yamekuwa yakifanyika,na kwa kweli si haba kazi inafanyika na kila mmoja anafanya wajibu wakeingawa siku zote tunaambiwa kila unapofanya moja unatakiwa uongeze jitihada zaidi lakini kwa ufupi tuseme kwamba kazi inafanyika vizuri"

  Ndugu hassan amesema mbali na vyombo hivyo kukabiliwa na majukumu makubwa ya utendaji wa kazi lakini waandishi wa habari hao wameweza kuitumikia vizuri serikali kwa kuelezea jitihada zinazochukuliwa na serikali kuwaletea maendeleo wananchi licha ya changamoto zinazowakabili.

  Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Habari maelezo Ndugu Hassan Vuai alisema ipo haja ya waandishi wa habari kuandika zaidi habari za maendeleo yanayofanywa na serikali vijijini.

  "Kila tunavyokuwa tunatoa elimu zaidi kupitia vyombo vyetu nafikiri ndio itakuwa tunawahamasisha zaidi.Tunasisitiza sana mtu kumkomboa kiuchumi ,mtu kumuendeleza kiuchumi.Sasa hivi kwa mfano vile visiwa vidogo vidogo ambavyo vimepatiwa umeme kwa mfano Fundo na kwengineko maeneo ya Pemba ukiwasikia wanavyozungumza utajua kwamba sasa wamefanikiwa hawa watu"

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako