• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya eneo la biashara huria Afrika kusainiwa nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-02-13 09:00:48

    Rais wa Rwanda ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Paul Kagame amesema makubaliano ya kihistoria kuhusu Eneo la Biashara Huria Barani Afrika yatasainiwa mwezi Machi mjini Kigali, Rwanda wakati wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika.

    Rais Kagame amesema makubaliano hayo yaliyoandaliwa kwa karibu miaka 40, yataleta maendeleo makubwa ya mafungamano na umoja. Amesema maendelo ya biashara huria ya Afrika yanayotarajiwa katika miaka ya mbele yatatoa fursa kwa makampuni ya Afrika kuingia kwenye ushindani na kushirikiana nje ya mipaka na hadi kufikia bara zima.

    Wakati huohuo naibu mjumbe maalumu wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika nchini Somalia Simon Mulongo amesema Umoja huo unaunga mkono watu kutembea kwa uhuru barani Afrika na utaendelea kushirikiana na jumuiya za kikanda kufikia malengo hayo. Amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza kasi ya mafungamano ya biashara na uchumi barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako