• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Riadha, Salome Nyirarukundo wa Rwanda ashinda nafasi ya tatu katika mbio za Barcelona

  (GMT+08:00) 2018-02-13 09:02:12

  Nyota namba moja kwa viwango vya ubora kwenye riadha kwa upande wa wanawake Nchini Rwanda Salome Nyirarukundo ameendeleza rekodi yake nzuri tangu mwaka huu uanze baada ya

  kushinda medali ya shaba kwenye mbio za kimataifa za Barcelona.

  Nyirarukundo alishinda tuzo hiyo kwa kushika nafasi ya tatu, alipotumia saa 1 dakika 8 na sekunde 48 kwenye mbio za mita 21,975, nyuma ya Tejitu Daba wa Bahrain aliyeshika nafasi ya kwanza na Dibabe wa Ethiopia aliyeshika nafasi ya pili.

  Kwa kutumia saa 1 dakika 8 na sekunde 48, Salome alifanikiwa kuvunja rekodi yake mwenyewe aliyoweka kwenye za Kigali alipotumia saa 1 dakika 13.

  Mwanariadha mwingine kutoka Afrika Mashariki aliyefanikiwa kukamata nafasi za juu ni Failuna Matanga wa Tanzania aliyekamata nafasi ya tano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako