• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchezaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta yaelezwa kuwa anaendelea vizuri kuuguza majeruhi

  (GMT+08:00) 2018-02-13 09:02:35

  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta inaelezwa kuwa anaendelea vizuri na alifanikiwa kufanya mazoezi kikamilifu na klabu yake, KRC Genk inayojiandaa na mechi ya Ligi Daraja la Kwanza dhidi Club Brugge Jumamosi ijayo.

  Hali ya Samatta iliingia utata alipoumia na kutolewa katika dakika ya 36 wakati wa mechi ya Genk dhidi ya Zulte Waregem, ambayo hata hivyo timu yake ilishinda kwa 3-1.

  Kwa mujibu wa daktari wa timu hiyo, majeraha hayo ni ya kawaida kwani huja na kupotea, hivyo yatakuwa yakipoa taratibu na hayawezi kumzuia kutocheza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako