• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi kuu ya nchinI Marekani; Lebron James aendelea kuwa msaada kwa timu yake ya Clevaland

  (GMT+08:00) 2018-02-13 09:03:29

  Ushindi wa alama 121-99 iliyoupata timu ya Cleveland Cavaliers dhidi ya Boston Celtic kwenye mechi ya jana, umeiongezea uhakika timu hiyo wa kushiriki robo fainali ya ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani ngazi ya kanda.

  Lebron James ndiye aliyekuwa chachu ya ushindi huo kufuatia ubora wa takwimu binafsi za kimchezo alizopata, akifunga alama 24, akimalizia ufungaji mara 10 na akitoa usaidizi mara 8.

  Wengine waliyochangia alama za Cleveland ni Jordan Clarkson 17, Rodney Hood 15, George Hill 12 na Larry Nance Jr. aliyefunga 5.

  Katika mechi inayofuata, Cleveland itakuwa na kibarua kizito dhidi ya Oklahima City Thunders usiku wa kuamkia kesho.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako