• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Klabu Bingwa Ulaya: Mechi za raundi ya 16 kuanza leo

  (GMT+08:00) 2018-02-13 09:03:53

  Mashindano ya ligi ya klabu bingwa barani Ulaya yanarejea tena leo usiku kwa hatua ya 16 bora ikiwa ni muda mrefu wa mapumziko kupita, ambapo jumanne hii kunachezwa mechi mbili za mzunguko wa kwanza katika nchi za Uswisi na Italia.

  Basel FC ya Uswisi itawakaribisha vinara wa ligi kuu nchini Uingereza Manchester City kwenye uwanja wa St. Jacob, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa timu hizo kukutana katika hatua hiyo, na Basel wakiwa na kiu kubwa ya kuwahi kufuzu robo fainali.

  Katika mechi nyingine itakayopigwa nchini Italia, wenyeji Juventus watakuwa na kibarua kizito cha kuizuia Tottenham ya Uingereza.

  Mzunguko wa marudiano wa mechi za leo utakuwa machi 7 mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako