• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Kuu ya Soka Uingereza; Ushindi wa Chelsea wampunguzia shinikizo kocha wa Antonio Conte

  (GMT+08:00) 2018-02-13 09:04:14

  Klabu ya Chelsea imefanikiwa kuishusha Tottenham kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza kufuatia ushindi wa magoli 3-0 kwenye mechi dhidi ya Westbrom Albion iliyopigwa jana usiku mjini London.

  Magoli mawili ya Eden Hazard yalichochea ushindi huo ambao sasa umeifanya timu hiyo ifikishe pointi 53, na goli lingine la tatu likifungwa na Victor Moses.

  Licha ya kuingia nne bora, ushindi huo umepunguza dhidi ya kocha mkuu wa timu hiyo Antonio Conte ambaye kuna uvumi kuwa huenda akafukuzwa kazi kufuatia matokeo mabaya ya timu hiyo.

  Ili kuonyesha kumuunga mkono kocha Conte, mashabiki wa Chelsea waliimba jina lake tangu mwanzo hadi mwisho wa mechi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako