• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uwekezaji wa China nje ya nchi waongezeka kwa miezi mitatu mfululizo

  (GMT+08:00) 2018-02-13 16:26:06

  Wizara ya Biashara ya China imesema mwezi Januari uwekezaji usio wa kifedha wa China katika nchi za nje ulifikia dola za kimarekani bilioni 10.8, ikiwa ni ongezeko la asilimia 39.7 na kutimiza ongezeko chanya kwa miezi mitatu mfululizo.

  Takwimu zilizotolewa na Wizara hiyo zinaonesha kuwa mwezi uliopita, wawekezaji wa kichina walifanya uwekezaji wa moja kwa moja usio wa kifedha kwa makampuni 955 katika nchi na sehemu 99 duniani. Kati ya hizo, uwekezaji ulifanywa katika nchi 46 zilizojumuishwa kwenye mpango wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuongezeka kwa asilimia 50 na kufikia dola za kimarekani bilioni 1.23.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako