• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kim Jong-un ataka kuweka mazingira zaidi kwa ajili ya mapatano na mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini

  (GMT+08:00) 2018-02-13 17:49:49

  Kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Kim Jong-un amesema ni muhimu kuendelea kuleta matokeo mazuri kwa kuweka mazingira zaidi kwa ajili ya mapatano na mazungumzo kati ya nchi yake na Korea Kusini.

  Kwa mujibu wa shirika la habari la Korea Kaskazini, Kim amesema hayo aliposikiliza ripoti ya ujumbe wa ngazi ya juu wa Korea Kaskazini uliorudi nchini mwao baada ya ziara ya siku tatu nchini Korea Kusini. Kim ameeleza kuridhika na kazi za ujumbe huo nchini Korea Kusini na pia kuishukuru Korea Kusini kwa kutilia maanani na kutoa urahisi kwenye ziara ya ujumbe wake.

  Aidha Kim amedhihirisha mwelekeo wa kuboresha na kuendeleza uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini katika siku za baadaye, na kuzitaka idara zinazohusika kuchukua hatua maalum katika suala hilo.

  Wakati huo huo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema suala la Peninsula ya Korea ni kiini cha tofauti kati ya Korea Kaskazini na Marekani, na China inatarajia nchi hizo mbili kutumia ipasavyo fursa nzuri zinazotokana na mawasiliano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini, na kupiga hatua zenye maana na kwa wakati.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako