• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chama tawala cha Afrika Kusini chamtaka rais Zuma kujiuzulu

  (GMT+08:00) 2018-02-13 17:55:42

  Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimempatia rais Jacob Zuma muda wa mwisho wa kujiuzulu ambao ni ndani ya saa 48 ama ataondolewa madarakani.

  Kamati Tendaji ya Taifa NEC ambacho ni chombo kikuu cha kufanya uamuzi wa chama hicho, inatarajiwa kumaliza suala hilo leo na kulitangazia taifa uamuzi wake, baada ya mikutano mfululizo iliyoendelea hadi jana usiku.

  Wataalamu wa sheria wamesema, kimsingi rais Zuma ameshaondolewa madarakani, lakini kamati ya NEC haiwezi kumfukuza. Kama rais Zuma akishikilia kuwepo na kukataa kujizulu, atalazimika kuondolewa madarakani kupitia kura ya kutokuwa na imani naye bungeni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako