• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakulima wa maua nchini Kenya walalamikia huduma isiyo na uhakika ya umeme

  (GMT+08:00) 2018-02-13 18:32:54

  Wakulima wa maua nchini Kenya wamelalamikia huduma ya umeme isiyo na uhakika katika eneo la Naivasha na kusema tatizo hilo linaathiri uzalishaji.

  Wakiongea kuelekea siku ya Wapendanao inayosherehekewa Jumatano, wakulima hao wamesema kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na wafanyakazi ni changamoto kubwa inayoikabili sekta hiyo hivi sasa.

  Kwa mujibu wa Meneja wa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Mawardi ya Van-Deng-Berg, George Onyango, awali walikuwa wakisafirisha mashina laki 5 ya mawardi kila siku nchini Ujerumani na Holand. Hata hivyo, Onyango anasema bei ya shina moja la waridi imesalia palepale kwa miaka mingi ikilinganishwa na kupanda kwa gharama za pembejeo za kampuni na usafirishaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako