• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Wakulima 36 wafidiwa na kiwanda cha mafuta Uganda

    (GMT+08:00) 2018-02-13 19:35:05

    Wakulima 36 nchini Uganda ambao ardhi yao ilitumiwa na kiwanda cha mafuta cha Bidco yamefidiwa.

    Fidia hiyo ilifuatia upatanisho ulioongozwa na shirika la fedha la kimataifa IFC lililoko chini ya benki ya dunia.

    Mwaka jana wanaharakati wa mazingira waliwasilisha keshi kwa IFC kwa niaba ya wakulima wa chama cha Bugala wakilalamika kwamba ardhi yao ilinyakuliwa na kiwanda hicho cha Bidco kimeharibu mazingira kwa ajili ya upanzi wa mitende.

    Ripoti ya baada ya kusuluhishwa kwa keshi hiyo inaonyesha kwamba wakulia 36 walifidiwa na wawili hawakuweza kupatikana.

    Hata hivyo kati ya hao 36, 8 walikataa makubaliano ya fidia na wanatarajiwa kuwasilisha kesi mahakamani baadaye mwezi huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako