• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirka ya ndege EAC yapiga hatua safari za ulaya na marekani

    (GMT+08:00) 2018-02-13 19:35:23

    Kampuni za ndege za Air Tanzania Limited (ATCL), Kenya Airways (KQ) na Rwandair zinatekeleza mikakati ya kujiimarisha ikiwa ni pamoja na kuanzisha safari za Ulaya, Marekani na Asia, kununua ndege mpya, na kusaini mikataba kukuza biashara.

    Julai mwaka huu, ATCL inatarajia kupokea ndege kubwa za abiria, ikiwemo aina ya Boeing 787 yenye uwezo wa kubeba abiria 262. Januari 17 mwaka huu, kampuni hiyo ilitangaza nafasi za kazi 88 za wahudumu kwenye ndege.

    Hatua hizo zimeelezwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa kuwa ni mchakato wa kuiboresha ATCL kwa lengo la kukuza biashara ndani na nje ya Tanzania kuliwezesha kuongeza mapato na kukuza uchumi wa taifa.

    Profesa Mbarawa alisema, ili kuiboresha ATCL, Serikali imeshanunua ndege mpya mbili aina ya Bombadier Dash 8-Q 400 zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja. Ndege hizo zimetengenezwa Canada, na ziliwasili nchini mwaka jana

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako