• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wadau wa kilimo walalamikia ugawaji na bei ya mbolea Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-02-13 19:35:41

    Kufuatia Mfumo wa Serikali Tanzania wa ununuzi na usambazaji wa mbolea (BPS), sasa wadau zikiwamo kampuni kubwa za ununuzi na usambazaji pamoja na wakulima, wanataka Serikali iwashirikishe kikamilifu.

    Baadhi ya mawakala wa mbolea mjini Makambako mkoani Njombe, wameeleza kusikitishwa na mfumo huo huku wakitaka kushirikishwa zaidi na Serikali ili kurahisisha upatikanaji wa mbolea.

    Mwenyekiti wa Agro Dealers katika Halmashauri ya Mji wa Makambako, Absalom Magoma anasema kumekuwa na upungufu wa mbolea ya kukuzia (Urea) na pia bei ya bidhaa hiyo ni ya juu.

    Magoma anasema bei hizo zimepangwa kwa maeneo ya mijini tu, mawakala wanaopeleka vijijini hawafaidiki nazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako