• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Bodaboda zina mapato makubwa Kenya

  (GMT+08:00) 2018-02-13 19:36:14

  Sekta ya waendeshaji pikipiki nchini Kenya maarufu maka doda boda inapata jumla ya shilingi bilioni 219 kila mwaka.mapato hayo ni yajuu ikilinganishwa nay ale ya kampuni kubwa zaidi Agfrika mashariki kwa mapato ya Safaricom ambayo inapata shilingi bilioni 212.

  Kulingana na taakwimu za chama cha watengenezaji pikipiki cha Afrika mashariki, kuna angalau pikipiki 600,000 kote nchini humo na huku kila mwendeshaji akipata dola 10 kwa siku, kwa mwaka inafikia shilingi bilioni 219.

  Mwenyekiti wa chama hicho Isaac Kalua amesema karibu watu 8 hutumia pikipiki moja kwa siku kwa shughuli zao za usafiri.

  Aidha taakwimu zinaonyesha kwamba pikipiki 146,000 zilinunuliwa mwaka 2016, kwa gharama ya shilingi bilioni 8.2.

  Pikipiki hutumika sana mijini ili kuepuka msongamano wa magari, na maendeo ya vijijini ambako hakuna usafiri wa mabasi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako