• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Radio inaweza kusaidia watu kutumia ipasavyo nguvu zao

    (GMT+08:00) 2018-02-14 07:55:39

    Tarehe 13 Februari ni Siku ya Kimataifa ya Radio. Katika maadhimisho ya siku hiyo, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema radio ni njia ya mawasiliano yenye nguvu na inayogharimu pesa kidogo, na inaweza kuwafikia watu wengi zaidi huku ikiwaunganisha watu kwenye michezo ya mashinani. Amesema redio inafaa zaidi kuzifikia jamii za mbali na watu wanyonge, wakiwemo watu wasiojua kuandika wala kusoma, wenye ulemavu na maskini. Ameongeza kuwa radio pia inaweza kutoa nafasi ya kushiriki kwenye mdahalo wa umma bila kujali ngazi ya elimu ya watu, na pia kuonesha nafasi yenye nguvu na maalumu katika mawasiliano ya dharura na uokoaji wa maafa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako