• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri barani Afrika watoa wito wa kuboresha sayansi ya anga za juu ili kusaidia usalama na maendeleo

    (GMT+08:00) 2018-02-14 08:04:06

    Mawaziri wa elimu ya juu na teknolojia ya mawasiliano barani Afrika wametoa wito wa matumizi ya kimkakati ya teknolojia ya sayansi ya anga za juu ili kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto zinazolikabili bara hilo ikiwemo umasikini, migogoro, magonjwa, na athari za mabadiliko ya hewa.

    Mawaziri hao wanaohudhuria Kongamano la Anga ya Juu ya Kimataifa unaofanyika mjini Nairobi, Kenya, wameeleza umuhimu wa sayansi ya anga ya juu kwa kufanya mabadiliko kwenye maisha ya jamii za bara la Afrika.

    Wabunge na wanasayansi waliohudhuria kongamano hilo wanatarajiwa kupitisha mkakati wa bara hilo wa kuleta uhai mpya kwenye ukuaji wa sayansi ya anga za juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako