• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mradi wa China kuwasaidia wakimbizi nchini Iran wamalizika

  (GMT+08:00) 2018-02-14 09:00:39

  Ubalozi wa China nchini Iran na ofisi ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP nchini Iran yamesaini hati ya makabidhiano mjini Tehran kuthibitisha kuwa mradi wa serikali ya China kuwasaidia wakimbizi wa Iraq na Afghanistan nchini Iran bila masharti umemalizika na kutimiza malengo yake.

  Kwa mujibu makubaliano yaliyosainiwa awali na serikali ya China na WFP, serikali ya China ilitoa dola za kimarekani milioni 1 bila masharti ili kutoa msaada wa chakula kwa wakimbizi walioko nchini Iran, na matumizi ya fedha na ununuzi wa chakula ulifanywa na WFP.

  Mjumbe wa WFP nchini Iran Bibi Negar Gerami ameshukuru msaada uliotolewa na China, na kusema fedha hizo zilitumika kununua tani 1200 za chakula na kuwasaidia wakimbizi elfu 30 nchini Iran.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako