• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Miji mikubwa ya China kukumbwa na wahudumu wa ndani katika kipindi cha sikukuu ya mwaka mpya wa jadi

  (GMT+08:00) 2018-02-14 17:06:07

  Miji mikubwa ya China kama Beijing inakabiliwa na upungufu wa wahudumu wa ndani baada ya wahudumu hao ambao wengi wao ni wafanyakazi wahamiaji kutoka mikoani, kusafiri kurudi makwao kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi.

  Gazeti la China Daily limeinukuu kampuni ya wahudumu wa ndani yenye wafanyakazi elfu 11 mjini Beijing, ikisema asilimia 95 ya wafanyakazi wake wamerudi makwao tangu mwanzoni mwa mwezi huu. Hata hivyo wachache waliobaki, wameamua kufanya hivyo kwa kuwa katika kipindi hicho wanalipwa mara mbili, ikilinganishwa ni kipindi cha kawaida.

  Ripoti iliyotolewa na wizara ya biashara ya China inaonyesha kuwa, mwaka 2016 watu milioni 26 walikuwa wanafanya kazi kwenye sekta ya uhudumu wa nyumbani, ikiwa imeongezeka kwa asilimia 9.3 kuliko mwaka uliotangulia. Pato kutokana na sekta hiyo linakadiriwa kufikia dola bilioni 52.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako