• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wasema mustakabali wa kisiasa wa rais Zuma hautaathiri mkutano wa wakuu wa nchi za BRICS

    (GMT+08:00) 2018-02-14 17:13:55

    Mchunguzi wa kituo cha utatuzi wa mgogoro mjini Cape Town Bw. Gwinyai Dzinesa, amesema kupunguzwa kwa uwezo wa rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini hakuwezi kuathiri mkutano wa kumi wa wakuu wa nchi za Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini utakaofanyika mwezi Julai mwaka huu.

    Chama tawala cha ANC kimemtaka rais Zuma ajiuzulu baada ya kufanya mazungumzo ya muda mrefu kuhusu hatma yake. Bw. Dzinesa amesema, kujiuzulu kwake hakuwezi kuathiri mkutano wa wakuu wa nchi za BRICS, kwani rais mpya wa Afrika Kusini ataitisha mkutano huo, na mpango uliopo utaendelea.

    Katibu mkuu wa chama cha ANC Bw. Ace Magashule, amesema, hapo awali rais Zuma aliomba muda wa miezi mitatu wa kujiuzulu bila masharti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako