• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Afghanistan yawakamata wafanyabiashara 14 wa magendo ya dawa za kulevya ndani ya wiki moja

  (GMT+08:00) 2018-02-14 18:17:18

  Polisi wa kupambana na dawa za kulevya wa Afghanistan wametoa taarifa wakisema wamewakamata wafanyabiashara 14 wa magendo ya dawa za kulevya kutoka mikoa tofauti nchini humo katika wiki iliyopita.

  Taarifa inasema dawa haramu zaidi ya tani moja, zikiwemo kilo zaidi ya 21 za heroin na kilo 200 za hashish zimekamatwa kutoka kwa watu hao, na kesi zao zinafanyiwa uchunguzi.

  Serikali ya Afghanistan imeimarisha mapambano dhidi ya biashara ya dawa za kulevya na imewahukumu watu wanane kifungo cha miezi sita hadi miaka miwili kutokana na kuhusika na magendo ya dawa za kulevya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako