• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uingereza imetoa vifaa vya kuzuia mambo ya msimamo mkali kwenye mtandao wa Internet

  (GMT+08:00) 2018-02-14 18:17:46

  Serikali ya Uingereza imetoa kifaa kinachoweza kuzuia kwa usahihi mambo kuhusu msimamo mkali kwenye mtandao wa Internet. Waziri wa mambo ya ndani ya Uingereza Bibi Amber Rudd, amesema kifaa hicho kipya kimetengenezwa na kampuni ya huduma ya data ya ASI inayowakilisha serikali ya Uingereza, na kinaweza kutambua na kuzuia asilimia 94 ya video za kundi la IS kwa usahihi wa asilimia 99.99.

  Bi Rudd amesema, kifaa hicho kimesanifiwa kwa ajili ya kampuni ndogo za teknolojia zisizoweza kulipia kubuni kifaa kama hicho. Lakini ametambua kuwa serikali haitazilazimisha kampuni za teknolojia kukitumia kwa mujibu wa sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako