• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa kilele wa shirika la SCO kufanyika mwezi wa Juni

  (GMT+08:00) 2018-02-14 18:18:30

  Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang, amesema China itafanya mkutano wa kilele wa shirika la ushirikiano la Shanghai SCO mwezi wa Juni huko Qingdao, mashariki mwa China. Russia ikiwa ni mwanachama muhimu wa shirika hilo, Rais wake amealikwa na China kuhudhuria mkutano huo.

  Balozi wa Russia nchini China Bw. Andry Denisov hivi karibuni amesema, rais wa Russia anatarajiwa kuhudhuria mkutano wa kilele wa Shirika la SCO. Kwa mujibu wa mila ya mawasiliano ya viongozi wa China na Russia, rais wa Russia ataweza kufanya ziara nchini China.

  Bw. Geng amesema, China inadumisha mawasiliano ya karibu na nchi wanachama kuhusu maandalizi ya mkutano huo wa kilele na kuharakisha uratibu. China itafanya juhudi za pamoja na pande mbalimbali husika, ili kuhimiza mkutano huo upate mafanikio.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako