• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uganda aishukuru China kwa kuunga mkono maendeleo ya Afrika

    (GMT+08:00) 2018-02-14 18:19:10

    Rais Yoweri Museveni wa Uganda ametoa shukrani kwa watu wa China kutokana na uuganji mkono unaoendelea kwa juhudi za nchi za Afrika katika kuleta uhuru wa kiuchumi wa nchi za Afrika.

    Rais Museveni alisema hayo alipokagua eneo la viwanda la Liaoshen huko Kapeeka lililojengwa na China akiambatana na balozi wa China nchini Uganda Bw. Zheng Zhuqiang. Amesema uungaji mkono wa China kwa nchi za Afrika umekuwa na historia ndefu sana.

    Rais Museveni amesema, wachina wameshirikiana na nchi za Afrika tangu wakati wa mapambano dhidi ya ukoloni. Marehemu Mao Zedong alianza kuziunga mkono nchi za Afrika hata wakati China iko nyuma kiuchumi.

    Pia amesema China inafanya kazi nyingi zaidi kuziunga mkono nchi za Afrika hasa Uganda. China pia inashirikiana na nchi za Afrika kwa ajili ya ustawi ya Pamoja. Rais Museveni pia ameipongeza China kwa kumaliza mwaka wa Jogoo na kukaribisha mwaka wa Mbwa kwa kalenda ya jadi ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako