• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Mapato ya kahawa yashuka kwa asilimia 13 kutokana na kushuka kwa bei za kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-02-14 19:23:50

    Mapato ya kahawa yameshuka kwa asilimia 13 katika miezi minne hadi Januri wakati bei za chini za kimataifa zimeathiri bei ya ndani.

    Ripoti ya soko la Kahawa la Nairobi imeonyesha kuwa mapato yalishuka kutoka Sh5.5 billion ($55) milioni mwezi Oktoba mwaka jana hadi Sh4.7 billion ($47 milioni) katika kipindi cha ukaguzi.

    Kahawa ya Kenya kwa kawaida huuzwa katika soko la kahawa la New York na mabadiliko yoyote ya bei huathiri mapato ya ndani.

    Bei hiyo ya chini ilisababishwa na kushuka kwa bei za kimataifa ambazo zilishuka hadi viwango vya chini katika miaka miwili kutoka viwango vya juu vya senti 150 kwa kila pauni hadi senti 120 .

    Bei ya wastani ilishuka kutoka Sh25,500 ($255) to Sh23,300 ($230) kwa kila mfuko wa kilo 50 uliouzwa katika mnada huo.

    Viwango vilivyotolewa kwa ajili ya kuuzwa pia vilishuka kwa asilimia 4 kutoka kilo milioni 10.8,wakati kushuka huko kukitajwa kuchangiwa na kucheleweshwa kwa bidhaa hiyo katika soko mwaka uliopita kutokana na hali mbaya ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako