• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Wakulima wadogo kunufaika na misaada ya IFAD

    (GMT+08:00) 2018-02-14 19:24:20

    Nchi wanachama 179 wa Shirika la Kimataifa la Misaada ya Maendeleo ya Kilimo (IFAD),wametangaza malengo ya kukusanya dola za Marekani bilioni 3.5 (tsh trilioni 7.8) kwa ajili ya mikopo na misaada ya kuboresha kilimo kwa wakulima wadogo wadogo milioni 47 wa vijijini.

    Miradi hiyo ni ile ya kupunguza umaskini na njaa kwa nchi zinazoendelea duniani,ikiwamo Tanzania.

    Rais wa IFAD Gilbert Houngbo alitangaza uamuzi huo juzi jijini Rome Italia wakati wa mkutano wa mwaka wa Baraza la Uongozi.

    Mkutano huo ulienda sambamba na mafunzo kwa wanahabari kutoka nchi 14 duniani juu ya uandishi wa habari za vijijini na kilimo.

    Tanzania ni miongoni mwa wanufaika wa miradi mbalimbali ya IFAD yenye lengo la kupunguza umaskini na njaa kwa ngazi ya kaya na wakulima wadogo wadogo tangu mwaka 1978.

    Aidha ilielezwa katika mkutano huo kuwa IFAD imeshatoa msaada wa dola za Marekani milioni 430.1 kwenye miradi 16 iliyonufaisha watanzania maskini wa kaya milioni nne.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako