• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda kutangaza uwezo wake katika mkutano unaoendelea wa kilimo cha maua

  (GMT+08:00) 2018-02-14 19:25:29

  Rwanda inalenga kutangaza uwezo wake kama mdau mkubwa katika sekta ya kilimo cha maua na mboga wakati wa mkutano wa siku mbili wa kilimo cha maua ambao umeanza leo jijini Kigali.

  Mkutano huo unalenga kujenga uhusiano kati ya Uingereza,Uholanzi na wadau wa ndani wa sekta ya kilimo cha maua na mboga.

  Waziri wa Kilimo na Rasilimali za Wanyama Gerardine Mukeshimana amesema mkutano huo unatoa fursa kubwa ya kuwatambulisha wawekezaji wa Uingereza na Uholanzi na wanunuzi wa mazao ya maua na mboga kwa wazalishaji na wasarishaji wa Rwanda.

  Mkutano huo ambao umevutia wawekezaji kutoka Uingereza,Uholanzi na Jumuiya ya Afrika Mashariki pia unatazamwa kama mwanzo wa uanzishaji biashara thabiti na fursa za uwekezaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako