• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Bodi ya Utalii kuitangaza Uganda kwa masoko mapya

    (GMT+08:00) 2018-02-14 19:25:54

    Katika juhudi za kuongeza idadi ya watalii,serikali ya Uganda inatafuta makampuni ya kimataifa ya mahusiano ya umma na masoko kuitangaza Uganda katika masoko mapya yanayojitokeza.

    Kulingana na taarifa kutoka Bodi ya Utalii Uganda (UTB),shirika la serikali la utangazaji utalii,masoko ymapya ambayo wanalenga ni pamoja na China,nchi za falme za kiarabu,Japan,nan chi za Nordic.

    Takriban shilingi bilioni 6 za Uganda zimeombwa kutoka kwa serikali ili kusaidia makampuni hayo mapya ya uhusiano wa umma na utangazaji pamoja na mengine matano ambayo yalipewa kazi hiyo miaka miwili iliyopita kuitangaza Uganda katika masoko yake ya jadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako