• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vikosi vya Kenya vyawaua magaidi watatu wa Al-Shabaab

    (GMT+08:00) 2018-02-15 16:42:55

    Askari wa Kenya wamewaua magaidi watatu wa kundi la Al-Shabaab katika operesheni ya usalama katika msitu wa Boni mjini Lamu.

    Msemaji wa Jeshi la Kenya Bw. David Obonyo amesema askari hao waliokuwa wakifanya doria walikutana na wapiganaji hao kufuatia mlipuko uliosikika Jumatano mapema. Amesema waliukuta mwili wa mpiganaji mmoja katika eneo la mlipuko wa bomu ambalo mpiganaji huyo alikuwa akipanga kutega kwenye barabara zinazotumiwa na askari.

    Baadaye askari hao walishambuliwa na kundi jingine la Al-Shabaab wakati wakiendelea na doria ili kusafisha eneo hilo, ambapo magaidi watatu waliuawa na wengine walikimbilia msituni wakiwa na majeraha. Askari hao walipata silaha, risasi na vifaa vya kutengezea mabomu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako