• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Egesho la kwanza katika bandari ya Lamu kukamilika mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-02-16 15:58:12

  Kampuni ya ujenzi ya China, China Communication Construction Company (CCCC) inatarajiwa kukamilisha egesho la kwanza la meli katika bandari ya Lamu katikati ya mwaka huu.

  Mradi huu, umetajwa kama mojawapo ya miradi mikubwa ambayo serikali ya Kenya inaendeleza kupitia ufadhili kutoka China.

  Mwandishi wetu wa Nairobi Serah Nyakaru ametuandalia ripoti ifuatayo.

  Ushirikiano baina ya Kenya na China unaendlea kuonekana, na hii nikupitia miradi kadhaa ambayo imepiga jeki uchumi wa Nchi na kubadilisha maisha ya wakazi.

  Mradi wa kwanza ambao umeleta mabadiliko mengi katika sekta ya usafiri ni reli ya sgr, ambayo sasa imesaidia katika kupunguza muda watu hutumia kusafiri kuenda Mombasa na Nairobi.

  Ukienda maeneo ya Lamu kuna mradi mkubwa ambao unaaminika kuwa kubwa Afrika Mashariki, na ni mradi wa Lapsset, ambao ni mradi mkubwa zaidia.

  Mradi huu, utakuwa na uwezo wa kuegesha meli kubwa kama vile meli ya panama.

  Bandari ya Lamu itakuwa na maeneo 32 ya kuegesha meli,huku ujenzi wa eneo la kwanza ukitarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka 2018.

  Mradi huu, wa Lappset unatarajiwa kugahrimu zaidi ya dola bilioni 26 kukamilika.

  Balozi wa China nchini Kenya, Liu Xianfa, hivi majuzi alizuru eneo la mradi huo, Lamu na kusema bandari hii, itatoa nafasi kubwa ya mizigo na mafuta

  "Bandari hii, itaonyesha maono ya Rais na Serikali yake. Ni naona ukuaji katika bandari ya Mombasa na, hivi karibuni hii bandari itakuwa na shughuli nyingi sana, kwa hivyo ni vyema kuwa na bandari kama hii kuweza kutoa nafasi nyingi za mizigo na pengine mafuta"

  Mradi wa Lappset ambao utaunganisha Kenya, Sudan Kusini na Ethiopia unatarajiwa kufungua nafasi elfu 424,800 kwa wakazi wa Lamu.

  Tayari kuna wale wamefaidika na mradi huu.

  Granton Mbanga ni mhandisi katika bandari ya Lamu.

  "Ni kubwa katika suala la urefu, ni karibu mita mia 400, itakuwa na uwezo wa kubeba meli kubwa kama vile panama, na pia itaimarisha biashara kati ya nchi za Afrika ya mashariki"

  Afisa Mkuu Mtendaji wa mradi wa LAPSSET,Silvester Kasuku anasema mradi huu mkubwa utaleta manufaa mengi nchini.

  "kutakuwa na biashara mbalimbali na viwanda vingi vitakavyotoa ajira kwa wakazi wa Lamu.Kutakuwa na ujenzi wa bomba la mafuta kutoka hapa hadi Sudan Kusini na Ethiopia"

  Aidha anasema ujenzi wa mradi wa LAPSSET na, kampuni ya China Communication Construction Company inatarajiwa kukamilisha ujenzi maegesho tatu ya kwanza ifikapo mwaka wa 2020 kwa gharama ya dola milioni 480.

  "Nadhani ni mradi mwingine mkubwa ambayo, kupitia ushirikiano wa Kenya na China tumefanya mradi huu kutimia. Na, ni matumaini yangu watu katika eneo hili la Lamu watafaidika"

  Bandari ya Lamu inatarajiwa kupita bandari ya Mombasa na kuwa bandari kubwa nchini Kenya na Afrika Mashariki katika miaka kumi ijayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako