• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Migogoro ya kimabavu ya Afghanistan yasababisha raia zaidi ya elfu 10 kuuawa na kujeruhiwa mwaka jana

    (GMT+08:00) 2018-02-16 16:58:52

    Ujumbe wa kutoa misaada kwa Afghanistan wa Umoja wa Mataifa (UNAMA) umetoa ripoti mjini Kabul, ukisema raia 3,438 wameuawa na wengine 7,015 wamejeruhiwa kutokana na migogoro na vurugu mbalimbali nchini Afghanistan mwaka 2017.

    Ripoti hiyo inahimiza pande zinazopambana nchini Afghanistan zichukue hatua zote zinazohitajika kuhakikisha usalama wa raia na kutoa wito kwa makundi ya upinzani kuacha kuwashambulia wananchi.

    Kiongozi wa ujumbe huo Bw. Tadamichi Yamamoto amesema ameshitushwa na idadi kubwa ya vifo vya raia kutokana na mashambulizi yaliyofanywa na makundi ya upinzani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako