• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yaimarisha usalama wa Tembo kwa kutumia Setilaiti

    (GMT+08:00) 2018-02-16 17:08:42

    Walinzi wa mazingira nchini Kenya wamesema wamewawekea alama tembo 20 kwa kutumia teknolojia ya setilaiti ili kufuatilia mwenendo wao, kupunguza migongano na kuimarisha hatua za usalama katika hifadhi ya Tsavo.

    Kundi la wanasayansi na watafiti na madaktari wa mifugo kutoka shirika la hifadhi ya wanyamapori la Kenya (KWS), kwa uungaji mkono wa shirika la Save the Elephants na mfuko wa hifadhi ya Tsavo, wamewawekea alama madume 10 na majike 10 kwa kutumia teknolojia za kisasa za ufuatiliaji.

    Kwa mujibu wa Shirika la hifadhi ya wanyamapori la Kenya, kufuatilia mwenendo wa Tembo hao kwenye hifadhi ya Tsavo, kutasaidia kukusanya taarifa muhimu za wanyama hao, kuhusu mienendo, mazingira yao na jinsi wanavyozoea miundo mbinu inayojengwa kwenye hifadhi hiyo, ili kuboresha uhifadhi wao na usimamizi kwenye eneo lao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako